Balozi Seif akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya CRJE inayojenga Jumba la Treni Darajani Bw. Li Yi katika Hoteli ya Kimataifa ya Sheraton Mjini Beijing Nchini China. Nyuma ya Bwana ni Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dr. Khalid Salum Mohamed.
Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya CRJE Bw. Li Yi akimueleza Balozi Seif nia ya Kampuni yake ya kutaka kuibadilisha Zanzibar kimajengo endapo itaendelea kupewa tenda za Ujenzi walipokutana Mjini Beijing China.
Ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ukiogozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ulioko upande wa Kulia ukifanya mazungumzo na Uongozi wa Shirika la Kimataifa linalotoa huduma za Kijamii la Nchini China la AVIC.
Balozi Seif wa Tatu kutoka Kulia na Ujumbe wake akiwa pamoja na Uongozi wa Avic International wa Nchini China ukiongozwa na Makamu wa Rais wa Shirika hilo Bw. Lin Jun kulia ya Balozi Seif mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Mjini Beijing.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya Uvuvi ya China ya Hongdon Bw. Lan Ping Yong Sheraton Hoteli Mjini Beijing China.
Balozi Seif akisalimiana na Makamu wa Rais wa Kampuni kubwa ya Miradi ya Umeme Duniani ya China Bwana Wang Pinshan kabla ya kuanza kwa mazungumzo yao kwenye Hoteli ya Kimataifa ya Sheraton Mjini Beijing.
Makamu wa Rais wa Kampuni kubwa ya Miradi ya Umeme Duniani ya China Bwana Wang Pinshan wa pili kutoka Kulia akikiongoza kikao cha mazungumzo ya pamoja na Ujumbe wa Zanzibar ulioongozwa na Balozi Seif wa Tatu kutoka Kushoto. Wa kwanza kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utawala Bora na Utumishi wa Umma Bibi Asha Ali Abdulla na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mh. Mohamed Ahmed Salum.Kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dr. Khalid Salum Mohamed na Katibu Mkuu wake Nd. Khamis Mussa.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Kampuni ya Kimataifa ya Uhandisi inayoshughulikia miradi ya Ujenzi wa Bandari na Madaraja Makubwa ya China { CHEC} iko tayari wakati wowote kuanzia sasa kusubiri kuanza kwa harakati za ujenzi wa Bandari ya Mizigo ya Mpiga Duri Mjini Zanzibar.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo Bwana Li Yi akiambatana na Timu ya wahandisi wa Kampuni hiyo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Ofisini kwake Mjini Beijing Nchini China.
Bwana Li Yi alisema Wataalamu na wahandisi wa Kampuni yake wameshakamilisha taratibu zote za kufanya Utafiti wa ujenzi huo baada ya kupewa nafasi hiyo kufuatia tenda iliyotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili ya Mradi huo.
Alieleza kwamba Kampuni hiyo kongwe Duniani iliyoasisiwa mwaka 1837 hivi sasa imebadilika kiutendaji ndani ya kipindi cha miaka miwili kwa kuzingatia zaidi sheria na taratibu wa Kimataifa kitendo chacho kimeleta mafanikio makubwa kwa Kampuni kiasi cha kuweza kuaminiwa na Taasisi na Mataifa tofauti Duniani..
Alisema Uwekezaji wa Kampuni hiyo Kimataifa umehamasisha kufungua Matawi yake kwa takriban Nchi 90 ambapo 30 kati ya hizo ziko Barani Afrika miongoni mwake zikiwemo Angola, Mzumbiji, Namibia, Afrika Kuisni, Zambia pamoja na Tanzania.
Akizungumzia Miradi mengine ya Uwekezaji ndani ya Kampuni hiyo Bwana Li Yi alimueleza Balozi Seif na Ujumbe wake kwamba Uongozi wa Kampuni hiyo umeamua pia kutekeleza baadhi ya miradi mengine kutokana na Taaluma na upeo mkubwa waliyonayo wahandisi wake.
Bwana Li Yi alisema CHEC kwa sasa ina uwezo wa kuendesha miradi ya Uvuvi, huduma za Maji, majengo ya bishara kubwa { MALL }pamoja na miundombinu ya miradi ya umeme na hata kilimo.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliufahamisha Uongozi wa Kampuni nhiyo ya CHEC kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haina pingamizi yoyote kwa uwamuzi wao huo wa kujihusisha na miradi mengine ya kiuchumi.
Balozi Seif alisema chakuzingatia zaidi katika miradi yao mipya wanayotaka kuianzisha ni kuandika barua za maombi na kuziwasilisha kwa Mamlaka inayohusika na Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar {ZIPA} kwa hatua zinazofaa.
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Ujumbe wake alifanya mazungumzo na Uongozi wa Kapuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya CRJE ya Mjini China chini ya Mwenyekiti wake wa Kanda ya Afrika Bwana Hu Bo.
Katika mazungumzo yao yaliyofanyika Hoteli ya Kimataifa ya Sheraton Mjini Beijing Bwana Hu Bo alisema Kampuni ya CRJE imeamua kuibadilisha Zanzibar kimajengo mazuri yakiwa na hadhi ya kisasa inayokubalika Duniani endapo wataendelea kukabidhiwa tenda za kazi hizo.
Mwenyekiti huyo wa CRJE Kanda ya Afrika alieleza kuwa Kampuni hiyo iliyokabidhiwa ujenzi wa Jumba la Treni Darajani inakusudia kulifanya Jengo hilo kuwa na hadhi ya hali ya juu wakizingatia uasili wake wa kihistoria.
Bwana Hu alisema pamoja na taratibu zilizowekwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni { Unesco } Kapuni yake itaheshimu pia usimamizi wa Mamlaka ya Mji Mkongwe wa Zanzibar uliopata hadhi ya kuwa miongoni mwa miji ya urithi wa hifadhi ya Kimataifa.
Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliyekiri uwezo mkubwa iliyonayo Kampuni hiyo ya Ujenzi ya CRJE baadaye mchana alionana kwa mazungumzo na Uongozi wa Kampuni Kubwa inayoongoza Duniani katika uendeshaji wa Miradi ya Umeme ya TBEA.
Balozi Seif aliueleza Uongozi huo wa TBEA chini ya Makamu wa Rais wake Bwana Wang Pinshan kwamba Wataalamu wa Taasisi hiyo wana fursa ya kuangalia namna wanavyoweza kuisaidia Zanzibar katika huduma mbadala ya nishati ya Umeme.
Balozi Seif alisema Visiwa vya Zanzibar kwa sasa vinatumia nishati hiyo ikiwa na kianzio kimoja tu kinachotokea Tanzania Bara bila ya kuwa na mbadala wake mwengine jambo ambalo linafaa kutafutiwa ufumbuzi wake.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuomba Uongozi wa Kampuni hiyo ya Umeme ya TBEA kutoa wataalamu wake kwa ajili ya kufanya utafiti wa kina katika miradi ya Umeme Visiwani Zanzibar.
Alieleza kwamba Utafiti huo baadaye unaweza kutoa muelekeo kwa Kampuni hiyo kuangalia mazingira yatakayoiwezesha kusaidia kupatikana kwa Umeme wa uhakika utakaokuwa mbadala endapo itatokea hitilafu kwa ule unaotumika kutoka Tanzania Bara.
Mapema Makamu wa Rais wa Kampuni ya Umeme ya TBEA Bwana Wang Pinshan aliueleza Ujumbe huo wa Zanzibar ukiongozwa na Balozi Seif kwamba wataalamu wa Taasisi hiyo wanaendelea kutumia Teknolojia mpya katika kuendesha miradi yao ya Umeme.
Bwana Wang alisema wakati tayari wameshatia nia ya kutaka kuwekeza miradi yao Zanzibar utekelezaji wa kazi zao unategemea zaidi mfumo wa Upepo, Maji, na Madini kama makaa ya Mawe.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Ujumbe wake walimalizia ziara yao Nchini Jamuhuri ya Watu wa China kwa kufanya mazungumzo na Uongozi wa Kampuni ya Uvuvi ya Hongdon chini ya mwenyekiti wao Bwana Lan Ping Yong.
Bwana Lan Ping katika mazungumzo yake alimueleza Balozi Seif kwamba ongezeko la Hoteli zilizopo Zanzibar hivi sasa zinahitaji kupata huduma za vyakula vya Baharini.
Alisema utafiti walioufanya katika kipindi kifupi cha ziara yao Visiwani Zanzibar imeonyesha wazi kwamba wavuvi waliowengi Zanzibar bado wanatumia zana duni za uvuvi zisizoweza kutosheleza mahitaji halisi ya walaji wa mazao ya baharini.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
23/12/2016.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni