Timu ya Chelsea inaongoza Kigi Kuu
ya Uingereza kwa tofauti ya pointi 9 ikijikita kileleni baada ya
kuifunga Bournemouth magoli 3-0 na kuweka rekodi ya kushinda michezo
12 mfululizo ya ligi hiyo.
Cesc Fabregas alimtengenezea goli
Pedro aliyetikisa nyavu kwa shuti la mpira uliobadili muelekeo na
kutinga kwenye kona ya juu ya goli, huku Eden Hazrad akifunga goli la
pili kwa mkwaju wa penati baada ya kuangushwa na Simon Francis.
Pedro aliongeza goli la tatu katika
muda wa majeruhi baada mpira walioupiga kwa shuti kali kumgonga Steve
Cook na mpira kukatiza kwenye mstari wa goli.
Mchezaji wa Chelsea Pedro akiachia shuti lililozaa goli
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni