Chelsea imefikia rekodi yake ya
kushinda michezo 11 ya Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kuifunga
Crystal Palace na kuongoza ligi hiyo kwa tofauti ya pointi tisa.
Katika mchezo huo Diego Costa
aliifungia Chelsea goli pekee katika jaribio la kwanza la
mashambulizi kwa mpira wa kichwa akiunganisha krosi ya Cesar
Azpilicueta.
Marcos Alonso karibu aongeze goli la
pili la wageni Chelsea baada ya mpira wa adhabu alioupiga kugonga
mwamba wa goli na kurudi ndani ya uwanja.
Diego Costa akiwa juu angani baada ya kuupiga mpira kwa kichwa uliozaa goli
Diego Costa akishangilia baada ya mpira wa kichwa alioupiga kujaa wavuni
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni