Mfanyabishara wa Meru nchini Kenya
ameangusha bonge la pati la kuwasili kwa gari lake jipya aina ya
Hammer H3 limousine, ambayo watu walidhani kuwa ni sherehe ya harusi
ya watoto wa matajiri.
Mfanyabishara huyo Zabron Mathenge
aliyenunua gari hilo kwa thamani ya shilingi milioni 40 za Kenya,
wakati wa kwenda kwenye sherehe hiyo alisindikizwa na bodaboda zote
za mji wa Meru.
Hata hivyo bodaboda hizo zilizoacha
shughuli zote za siku hiyo ili kulisindikiza gari lake hilo la Hammer
H3 aliloagiza kutoka Marekani, madereva wake waliambulia shilingi
1,000 ya Kenya kila mtu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni