(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano-WFM)
Alhamisi, 8 Desemba 2016
JAPAN YAAHIDIKUENDELEA KUISAIDIA TANZANIA KUIMARIKA KIUCHUMI
Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bi. Noriko Suzuki (kulia), akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo Pichani), alipomtembelea na kufanya mazungumzo naye Ofisini kwake Jijini Dar es salaam. Katikati ni Mwakilishi Mkuu Mkazi wa JICA nchini Tanzania, Bw. Toshio Nagase na kulia ni Afisa wa Shirika hilo anayeshughulikia masuala ya usafiri na usafirishaji Bi. Lilian Masalu.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (wa pili kulia), akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumzia umuhimu wa Nishati ya umeme katika kuchochea maendeleo ya viwanda nchini, wakati alipokutana na Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) Bi. Noriko Suzuki, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia), akizungumzia namna Serikali ya Tanzania ilivyojipanga kutekeleza miradi mbalimbali ya kipaumbele ikiwemo ujenzi wa viwanda mbele ya Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Bi. Noriko Suzuki (hayupo pichani), alipomtembelea na kufanya naye mazungumzo ofisini kwake Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Sheria Bw. Elias Kalist, na kulia kwake ni Mchumi Mkuu, Yosephe Tamamu, wote kutoka Wizara ya Fedha na Mipango.
Mchumi Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Yosephe Tamamu (kushoto), akifafanua jambo katika kikao kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) na Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) Bi. Noriko Suzuki. Aliyekaa kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Sheria wa Wizara hiyo Bw. Elias Kalist.
Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) Bi. Noriko Suzuki, akizungumza katika kikao na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani), kuhusu ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Japan, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akimsindikiza mgeni wake, Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) Bi. Noriko Suzuki, baada ya kufanya mazungumzo namna pande hizo mbili zitakavyoimarisha ushirikiano uliodumu muda mrefu katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (kulia) akifurahia jambo na mgeni wake, Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) Bi. Noriko Suzuki, kabla ya kuondoka baada ya kufanya mazungumzo namna pande hizo mbili zitakavyoimarisha ushirikiano uliodumu muda mrefu katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii. Kulia ni Mwakilishi Mkuu mkazi wa JICA hapa nchini, Toshio Nagase.
(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano-WFM)
(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano-WFM)
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni