.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 19 Desemba 2016

KONGAMANO LA VILABU VYA UMOJA WA MATAIFA UN LAFANA TANGA



Tanga, WANAFUNZI wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa kutoka vyuo Vikuu na Shule za Sekondari na Msingi kutoka Mikoa mbalimbali nchini wamekutana Tanga kujadili mambo mbali mbali yahusuyo shughuli za Umoja wa Mataifa.
 

Wanafunzi hao walijadili mambo hayo yakiwemo Demokrasia na Utawala bora Barani Afrika pamoja na changamoto za Raia katika nchi zenye machafuko.
Pia walijadili uchafuzi wa mazingira kwa nchi zenye viwanda na uharibifu wa mazingira ya bahari kwa baadhi ya viwanda kumwaga sumu baharini.

Akizungumza katika kongamano hilo, Mlezi wa (YUNA) Mkoa wa Kilimanjaro, Fransiss Shelutete, amezitaka Serikali nchi za Afrika kuwachukulia hatua kali uchafuzi wa mazingira

Mwenyekiti wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa (YUNA) nchini Rahim Nassir, akizungumza kwenye kongamano la vilabu vya umoja wa Mataifa lililowashirikisha wanafunzi vyuo vikuu na kufanyika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Wanachama wa vilabu vya Umoja wa Mataifa (YUNA) kutoka Mikoa mbalimbali nchini wakifuatilia kongamano lililohusisha wanafunzi wa vyuoni na Shule za Sekondari na Msingi na kufanyika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Tanga
Viongozi wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa UN kutoka Mikoa mbalimbali nchini wakiwa katika picha ya pamoja na wanachama kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Mratibu wa klabu ya Umoja wa Mataifa (YUNA) Mkoa wa Kilimanjaro, Fransisis Shelutete, akizungumza kwenye kongamano la Vilabu vya Umoja wa Mataifa kutoka Mikoa mbalimbali nchini na kufanyika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Tanga. Blog ya kijamii tangakumekuchablog 0655 902929

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni