Lionel Messi amekutana na mtoto wa
kiume raia wa Afghanistan ambaye alitengeneza mfuko wa
plastiki kama fulana ulioandikwa Messi 10.
Messi amekutana na mtoto huyo
Murtaza Ahmadi, jana katika mchezo wa kirafiki na Al-Ahli ambao
Barcelona ilishinda kwa magoli 5-3, nchini Qatar.
Katika mchezo huo Lionel Messi, Luis
Suarez na Neymar wote walitikisa nyavu wakati Barcelona ikiifunga
Al-Ahli huko Qatar.
Mtoto huyo mwenye umri wa miaka sita
alipata umaarufu baada ya picha yake kuwekwa kwenye mitandao ya jamii
akiwa na jezi hiyo ya nyota wake ampendaye.
Dogo akiwa amepozi na jezi yake ya Lionel Messi aliyoitengeneza kwa kutumia mfuko wa plastiki
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni