Timu ya Arsenal imemaliza Ligi ya
Mabingwa Ulaya hatua ya makundi kwa kuwa ya kwanza katika kundi A,
baada ya kuifunga Basel magoli 4-1 huku magoli matatu yakifungwa na
Lucas Perez.
Ushindi huo umeifanya Arsenal
kuipiku Paris St-Germain iliyotoka sare ya magoli 2-2 dhidi ya Ludogorets Razgrad, katika mchezo
ambao ambao walikuwa wanahitaji ushindi wa aina yoyote ule ili
kuongoza kundi hilo.
Lucas Perez alifunga goli la kwanza
katika dakika ya nane na kuongeza la pili dakika ya 16 kabla ya
kuhitimisha hat-trick yake katika dakika ya 57. Alex Iwobi alifunga
goli la nne kabla ya Seydou Doumbia kufunga goli pekee la
Basel.
Lucas Perez akifunga goli lake la pili katika mchezo huo
Katika mchezo mwingine Manchester
City ambayo imeshajihakikisha kutinga hatua ya mtoano katika ligi ya
Mabingwa Ulaya ilijikuta ikilazimika kuchomoa goli na kutoka sare ya
1-1 na Celtic katika dimba la Etihad Stadium.
Celtic ilipata goli lake kupitia
mchezaji anayecheza kwa mkopo winga Patrick Roberts katika dakika ya
nne tu ya mchezo kwa kumalizia vizuri pasi aliyopewa, lakini furaha
yao ilidumu kwa dakika nane tu kabla ya Kelechi Iheanacho
kusawazisha.
Patrick Roberts akiwa amemzidi maarifa kipa Willy Caballero
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni