Rais wa Cuba Raul Castro ameongoza
tukio la mwisho la kumuenzi kaka yake marehemu Fidel Castro
lililofanyika katika mji wa Santiago.
Makumi ya maelfu wananchi wa Cuba
walihudhuria tukio hilo pamoja na viongozi kadhaa wa dunia.
Akiongea katika tukio hilo Raul
Castro ameapa kulinda misingi ya kisosholisti na malengo yake
yaliyoongozwa na Fidel, aliyefariki dunia Novemba 25, akiwa na umri
wa miaka 90.
Pia ametangaza kuwa Cuba itapiga
marufuku kuita jengo lolote ama barabara jina la Fidel Castro ikiwa
ni ombi alilotoa marehemu kaka yake kabla ya kufa.
Majivu ya mwili wa kiongozi wa mapinduzi ya Cuba Fidel Castro yakiwa yamebebwa kwenye kisanduku chenye bendera kwenye gari maalum la jeshi
Mmoja wa wapiganaji wakati wa mapinduzi Paulina Bellard akiangua kilio baada ya kuona sanduku lenye majivu ya mwili wa Fidel Castro
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni