.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 8 Desemba 2016

MHE. KAIRUKI NA BALOZI WA JAPANI NCHINI WAFANYA MAZUNGUMZO KUHUSU USHIRIKIANO KATI YA TANZANIA NA JAPANI

kai
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Balozi wa Japani nchini Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida (hayupo pichani) alipomtembelea ofisini kwake leo kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Japani hususan suala la wataalamu wa kujitolea wanaokuja kufanya kazi nchini katika sekta mbalimbali.
kai-1
Balozi wa Japani nchini Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida (kushoto) akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (hayupo pichani) alipomtembelea ofisini kwake leo kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Japani hususan suala la wataalamu wa kujitolea wanaokuja kufanya kazi nchini. Kushoto kwake ni Afisa wa Ubalozi wa Japani nchini, Bi. Yoko Kamiyana.
kai-2
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (wa pili kulia) akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaharu Yoshida (wa pili kushoto) alipomtembelea ofisini kwake leo kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Japani hususan suala la wataalam wa kujitolea wanaokuja kufanya kazi nchini katika sekta mbalimbali.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni