.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 3 Desemba 2016

MIILI YA WACHEZAJI WA TIMU YA CHAPECOENSE KUPOKELEWA LEO BRAZIL

Miili ya watu 71 waliokufa katika ajali ya ndege nchini Colombia, na kuleta majonzi kwa soka la taifa la Brazil na dunia kwa ujumla inarejeshwa nyumbani kwa ajili ya maziko.

Zaidi ya watu 100,000 wanatarajiwa kujitokeza kwa ajili misa maalum itakayofanyika kwenye uwanja wa Chapeco baadaye hii leo.

Watu sita tu walinusurika kifo siku ya jumatatu, katika ajali hiyo nje ya mji wa Medellin, wakati wachezaji wa timu ya Chapecoense walipokuwa wanaenda kucheza mchezo wa fainali.

Rais wa Brazil Michel Temer anatarajiwa kuwapo uwanja wa ndege kuipokea miili ya wachezaji wa timu ya Chapecoense itakapowasili kwa ndege.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni