Mwenyekiti wa Wanawake Wafanyabiashara katika Soko hilo, Betty Mtewele (kushoto), akisisitiza jambo kwenye uzinduzi huo.
Wananchi waliohudhuria uzinduzi huo.
Wadau wa EfG wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wadau wa EfG wakiwa wakiwa katika picha ya pamoja mgeni rasmi wa Diwani wa Kata ya Mchikichini, Joseph Ngowa (kushoto)
Diwani wa Kata ya Mchikichini, Joseph Ngowa (kushoto), akigawa vipeperushi vya kupinga ukatili wa kijinsia kwa wafanyabiashara wa soko la Mchikichini.
Wasanii wa kundi la machozi wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wasanii wa Kikundi cha Machozi wakitoa burudani kwenye uzinduzi wa kampeni ya siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia ulioandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG) uliofanyika Soko la Ilala Mchikichini Dar es Salaam leo.
Uzinduzi ukiendelea
Wasaidizi wa kisheria masokoni, Aisha Juma (kushoto) na Irene Daniel wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Usikivu kwenye uzinduzi huo. Katikati ni Msaidizi wa kisheria masokoni Batuli Mkumbukwa.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi Diwani wa Kata ya Mchikichini, Joseph Ngowa.
Na Dotto Mwaibale
DIWANI wa Kata ya Mchikichini Joseph John Ngowa (Chadema), amemfutia leseni ya biashara, Alex Richard muuza mitumba katika Soko la Karume Ilala jijini Dar es Salaam baada ya kumbamba akimfanyia udhalilishaji mteja wake wa kike.
Tukio hilo limetokea Dar es Salaam leo mchana wakati Diwani huyo alipokuwa akienda kugawa vipeperushi vya kupinga ukatili wa kijinsia kwa wafanyabaiashara wa soko hilo baada ya kuzindua kampeni ya siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyoanzishwa na Shirika la Equality for Growth (EfG) ndipo alipoingia kwenye kibanda cha mfanyabiashara huyo na kumkuta mteja wa kike akiwa ametoa nguo zake akipimishwa nguo za mitumba kitendo ambacho ni ukiukaji wa sheria ndani ya soko hilo.
“Kuanzia leo hii naagiza ufutiwe leseni yako ya biashara kutokana na tukio ili la aibu na kidhalilishaji ili iwe fundisho na kwa wengine” aliagiza Ngowa.
Ngowa alitishia kuwafuti leseni za biashara wafanyabiashara watakaobainika kuwadhalilisha wateja wao hasa wanawake na kuwa wanamsaka kijana moja maarufu kwa jina la Kipracheche ambaye ni kinara wa ubakaji na kudhalilisha wanawake katika soko hilo ikiwa ni pamoja na kulisambaratisha kundi la kihalifu sokoni hapo linalojulikana kwa jina la Masabanga.
Mfanyabiashara huyo Alex Richard alipohojiwa na wanahabari kuhusu vitendo hivyo aliomba samahani na kuwataka wenzake waache kufanya vitendo hivyo vya udhalilishaji kwa wanawake.
Mwenyekiti wa Wanawake Wafanyabiashara katika Soko hilo, Betty Mtewele alisema mfanyabiashara yeyote atakaye bainika kujihusisha na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia hata unewa huruma atachukuliwa hatua kazi za kisheria.
Akizungumza katika uzinduzi huo Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Shabani Rulimbiye alisema katika vitendo vya kupinga ukatili wa kijinsia shirika hilo linaendesha mradi unaoitwa “Mpe Riziki si Matusi” katika Wilaya ya Ilala na Temeke katika masoko sita ambayo ni Mchikichini, Kisutu, Tabata Muslimu, Ferry, Gezaulole na Temeke Sterio lengo likiwa ni kuona wanawake wafanyabiashara wa Manispaa ya Ilala na Temeke wanafanyabiashara zao katika mazingira huru dhidi ya ukatili wa kingono, kimwili, matusi na kisiasa, vilevile kuona wanawake wakipewa heshima kama binadamu wengine ili waweze kujipatia kipato chao bila vikwazo.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni