Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
akizungumza na na vijana wa vikundi mbalimbali vya michezo (hawapo pichani) walivyoshiriki katika matembezi ya kupinga Udhalilishaji wa Wanawake na Watoto ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Haki Za Binadamu. Tukio hilo liliandaliwa na Baraza la Taifa la Vijana, Zanzibar na lilifanyika Mnarani Mwembe Kisonge, mjini Unguja, Zanzibar. Katika hotuba yake, Masauni alisema matukio ya unyanyasi yanaongezeka kwa wingi nchini, hivyo amewataka wananchi kujitokeza kutoa taarifa za ukatili na unyanyasaji katika vyombo husika kwa wakati. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati waliokaa), Mwenyekiti wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC), Prof. Chris Maina Peter (wapili kushoto waliokaa), Mkurugenzi wa Kituo wa Kituo hicho, Harusi Miraji Mpatani (wa pili kulia waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani. Masauni alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa ZLSC, mjini Unguja, Zanzibar. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni