Mkuu wa mradi wa Agra, ambaye pia ni
Mhadhiri katika Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini-Dodoma, Dkt.
Mark Msaki (kushoto), akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (Katikati) wakati akikagua
maonesho ya taaluma, huduma na bidhaa kabla ya kutunuku tuzo
mbalimbali kwa wahitimu 829 katika Mahafali ya 30 ya Chuo Cha Mipango
ya Maendeleo Vijijini, Kituo cha Mwanza. Kushoto kwa Dkt. Kijaji na
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina
Mabula (Mb).
Mwanafunzi wa kike wa Stashahada
Mwaka wa Pili wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kituo cha
Mwanza, akielezea kuhusu mafunzo wanayoyapata chuoni hapo na namna
elimu hiyo inavyosaidia kuendeleza vijiji walivyokwenda kufanya
mazoezi kwa vitendo mkoani Mwanza, wakati Naibu Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) alipotembelea na
kukagua maonesho hayo ya taaluma, huduma na bidhaa zinazotolewa na
chuo hicho.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto), akionesha moja ya machapisho
yaliyotolewa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini wakati
alipotembelea na kukagua maonesho ya taaluma, huduma na bidhaa kabla
ya kutunuku tuzo mbalimbali kwa wahitimu 829 katika Mahafali ya 30 ya
Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kituo cha Mwanza.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto), akisikiliza kwa makini
maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkufunzi wa Chuo cha Mipango na
Maendeleo Vijijini Bw. Ezekiel Kanire, (aliyeshika kipaza sauti)
wakati alipotembelea na kukagua maonesho ya taaluma, huduma na bidhaa
kabla ya kutunuku tuzo mbalimbali kwa wahitimu 829 katika Mahafali ya
30 ya Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kituo cha Mwanza.
Kushoto kwa Dkt. Kijaji na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula (Mb).
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto), akiangalia kipeperushi chenye
maelezo ya faida za kutumia kitunguu swaumu kwa binadamu wakati
Mkulima wa zao la vitunguu swaumu kutoka Wilayani Mbulu Mkoani
Manyara, Bw, Boniface Bura, (aliyeshika kipaza sauti), akitoa maelezo
namna Chuo chas Mipango ya Maendeleo Vijijini kilivyomsaidia kuongeza
thamani ya zao hilo, wakati Naibu waziri huyo alipotembelea na
kukagua maonesho ya taaluma, huduma na bidhaa zinazotolewa na Chuo
cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kituo cha Mwanza.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto), akipokea zawadi ya Kitunguu
swaumu kilichosindikwa, kwaniaba ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe
Magufuli iliyotolewa na Mkulima wa zao hilo kutoka Wilayani Mbulu
Mkoani Manyara, Bw. Boniface Bura, anayenufaika na mradi wa
kuwawezesha wakulima vijijini wa Mivaraf, ikiwa ni ishara ya kuunga
mkono Jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano ya Viwanda.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto), akizungumza na vyombo vya
habari baada ya kumaliza kutembelea na kukagua maonesho ya taaluma,
huduma na bidhaa kabla ya kutunuku tuzo mbalimbali kwa wahitimu 829
katika Mahafali ya 30 ya Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini,
Kituo cha Mwanza.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni