Timu za Taifa za umri chini ya miaka 23 kwa wanaume na wanawake ambazo hazikuwa na majina sasa zinaitwa Kilimanjaro Warriors (wanaume) wakati wanawake ni Kilimanjaro Starlets.
Uteuzi wa majina hayo umefanywa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao chake kilichofanyika jana (Desemba 17, 2016) jijini Dar es Salaam.
Timu hizo ambazo ni maalumu kwa ajili ya michuano ya Olimpiki zitaanza maandalizi yake Januari mwakani, na wengi wa wachezaji watakaounda timu hizo zinazojiandaa kwa ajili ya michuano ya Olimpiki itakayofanyika Tokyo, Japan mwaka 2020 watatoka katika timu za sasa za wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 (U20).
Mechi za mchujo (qualifiers) kwa ajili ya michuano ya Olimpiki ya 2020 zitaanza mapema mwaka 2019.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni