Mwanamke mmoja nchini Australia
amebaini uwepo wa nyoka mwenye urefu wa mita moja ambaye amejificha
kama pambo kwenye mti wake wa Krismasi.
Mwanamke huyo alilazimika kupiga
simu kuomba msaada wa kuondolewa kwa nyoka huyo kwenye nyumba yake
huko Melbourne, Victoria, siku ya jana.
Mtaalam wa kushika nyoka Barry
Goldsmith amesema nyoka huyo aliingia mlangoni na kisha
kujiviringisha kwenye mti wa Krismasi kama pambo.
Nyoka huyo aina ya Tiger, ambaye
anapatikana nchini Australia huwa na sumu kali sana.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni