Rais Barack Obama ameapa kuchukua
hatua dhidi ya Urusi kutokana na tuhuma za kuhusika katika kuingilia
kampeni za uchaguzi wa Marekani.
Urusi imekuwa ikituhumiwa kufanya
udukuzi wa barua pepe za Chama cha Democratic pamoja na wasaidizi
muhimu wa Bi. Hillary Clinton, tuhuma ambazo imezikanusha vikali.
Rais Mteule wa Marekani Donald Trump
pia amekanusha madai hayo kwa kusema ni ya kipuuzi na yamechochewa
kisiasa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni