Rais wa Gambia Yahya Jammeh amekataa
matokeo ya uchaguzi ya urais uliofanyika mwezi huu, ikiwa ni wiki
moja tu tangu akubali kushindwa.
Jammeh ameelezea sababu za kukataa
matokeo hayo kuwa ni kuwapo kwa hitilafu katika upigaji kura na
kutaka kuitishwa uchaguzi upya.
Jammeh, aliyeingia madarakani baada
ya mapinduzi ya mwaka 1994, alishindwa na mpinzani wake Adama Barrow,
ambaye alishinda kwa kura asilimia 43.
Bw. Barrow amemtuhumu rais
aliyemadarakani kwa kuvunja demokrasia kutokana na kutokubali
matokeo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni