Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemteua Bi. Aziza Badru Mwanje kuwa Mkurugenzi mpya wa Fedha na Utawala kuanzia Januari Mosi, 2017.
Uteuzi huo umefanywa (Desemba 17, 2017) na Kamati ya Utendaji ya TFF kufuatia mchakato wa usaili uliohusisha waombaji wengine wawili na kufanywa na Bodi ya Ajira ya TFF.
Vilevile Kamati ya Utendaji imefanya mabadiliko ya wajumbe katika Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ambapo Wakili Patrick Sanga atakuwa Makamu Mwenyekiti wakati Mwenyekiti anaendelea kuwa Wakili Richard Sinamtwa.
Wajumbe wengine walioongezwa kwenye Kamati hiyo ni Bw. Adam Mihayo na Bw. Hassan Hassanoo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA).
Wakili Raymond Wawa ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF kuziba nafasi ya Bw. Joseph Mapunda ambaye ameomba kupumzika.
Pia Bibi Mia Mjengwa ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni