.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 2 Desemba 2016

VIJANA WAKUBALI MAENDELEO ENDELEVU, WAAHIDI KUYAPELEKA VIJIJINI

Wakati wanachuo wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha mjini Mbeya wakiahidi kupeleka vijijini kampeni ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez amesema kwamba utekelezaji wa malengo hayo uko mikononi mwa vijana zaidi.

Alisema nchini Tanzania zaidi ya nusu ya watu wake ni vijana hivyo wakielewa malengo hayo itakuwa rahisi kushawishi wengine kuhuisha maendeleo hayo na shughuli zao za kila siku huku wakitunza mazingira.

Alisema shauri kwanini malengo yamekuwa mengi wakati yale ya Milenia yalikuwa nane tu, Mratibu huyo alisema kwamba suala si uwingi wa malengo bali maana yake na haja ya utekelezaji.
img_3409
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya, Dr. Daniel Mosses akimkaribisha na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyemtembelea ofisini kwake mjini Mbeya.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

Alisema MDGs (Malengo ya Millennia) iliacha masuala kadhaa bila uelekeo ikiwamo suala la mazingira na mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kuwapo kwake kunahakikisha uwapo wa maendeleo endelevu kwa kuwa kila kitu kinategemea sana mabadiliko ya tabia nchi kwa sasa.

Alisema ni matumaini yake kwamba kuzinduka kwa jamii ya vijana itasaidia kukabiliana na changamoto hizo za sasa za dunia.

Kauli ya mratibu huyo iliungwa mkono na wanachuo hao ambao walisema kwamba wanaona uhalisia wa mahitajhi ya sasa na kwamba watawasilisha kampeni hiyo maeneo wanayotoka ili kuwapo na mabadiliko.
img_3418
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya, Dr. Daniel Mosses akiwa kwenye mazungumzo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mtaalam wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu.

Kwa kuwa wengi ni vijana na kwa kuwa asilimia 75 ya vijana wanaishi vijijini, itakuwa heri kama walivyofundishwa na Umoja wa Mataifa kupeleka salamu vijijini ili kukabiliana na tatizo la mazingira na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanafumua misimu ya kilimo na upatikanaji wa mvua.

Kushirikisha vijana ni suala la msingi sana, hasa ikizingatiwa kwamba sehemu kubwa ya vijana wanatoka vijijini ambako malengo ya maendeleo endelevu yana maana zaidi kwa umma, alisema Kidai Kabula Shaban, Mwanafunzi anayesomea Shahada ya Sanaa, Sosholojia na Kazi za Jamii.
img_3474
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya, Dr. Daniel Mosses akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez kuendesha semina ya malengo ya dunia (Global Goals) kwa wanafunzi wa chuo hicho iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).

Amesema amefurahishwa mno na mpango huo wa kuelimisha vijana hasa utunzaji wa mazingira ili kukabiliana na tabia nchi. Alisema yeye alivyoelimishwa basi atahakikisha anawaelimisha wengine kuwa watekelezaji wa maendeleo hayo. Akirejea mazungumzo ya mwanafunzi huyo kwa niaba ya wenzake.

Alvaro alisema amefurahishwa na mwamko wa vijana wa kutaka kujua malengo hayo na ni imani yake kwamba kwa kuwakujua wao basi jamii itaerevuka mapema zaidi.
img_3492
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendesha semina kuhusu malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
img_3500
img_3544
Mtaalam wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu akiwapiga msasa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji jijini Mbeya wakati wa semina kuhusu malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
img_3554
Mtaalam wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu akifafanua jambo wakati wa semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji jijini Mbeya iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
img_3579
Mwalimu wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji cha jijini Mbeya, Furaha Komoro akiuliza swali kuhusu juhudi za Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha usawa wa kijinsia unakuwa na uwiano sawa pande zote.
img_3597
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji akishiriki kutoa maoni kwenye semina ya malengo ya dunia iliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa na kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
img_3570
Mwanafunzi anayesomea Shahada ya Sanaa, Sosholojia na Kazi za Jamii chuoni hapo, Kidai Kabula Shaban akiuliza swali kwa mkufunzi (hayupo pichani) wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).
img_3437
Pichani juu na chini ni sehemu ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji jijini Mbeya walioshiriki semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
img_3452
img_3458
img_3461
img_3464
img_3511
img_3443
Mmoja wa washiriki akipitia kijarida cha malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) katika semina iliyofanyika Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji jijini Mbeya.
img_3614
Picha juu na chini ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji cha jijini Mbeya waliohudhuria semina ya malengo ya dunia (Global Goals) iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
img_3631
img_3632
Pichani juu na chini ni semina maalum ya mabalozi wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs Champions/Global Goals Champions) wakipigwa msasa wa SDGs na Mtaalam wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu (hayupo pichani).
img_3636
img_3733
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akikabidhi cheti kwa Balozi wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (Global Goals Champion) Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) ambaye pia ni mrembo wa taji la Miss Mbeya 2016, Eunice Robert.
img_3767
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akikabidhi cheti kwa Balozi wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (Global Goals Champion) Rais wa serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya, Mahona Byura.
img_3682
Picha juu na chini ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akikabidhi cheti kwa baadhi ya Mabalozi kati ya 50 wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (Global Goals Champion) katika Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji cha jijini Mbeya.
img_3702
img_3722
img_3736
img_3748
img_3755
img_3766
img_3793
img_3795
img_3798
img_3830
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na mabalozi wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) Global Goals Champions wakiwa wameshikilia vyeti vyao mara baada ya kuhitimisha semina maalum kwa mabalozi hao.
img_3835
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na mabalozi wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) Global Goals Champions wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya wakiwa wameshikilia baadhi ya SDGs.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni