.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 5 Desemba 2016

WAGONJWA WA AKILI 100 WATOROKA WAKATI MGOMO WA MADAKTARI KENYA UKIANZA LEO

Operesheni kubwa imeanzishwa nchini Kenya kufuatia wagonjwa wa akili zaidi ya 100 kutoroka katika hospitali ya wagonjwa wa akili ya Mathari Jijini Nairobi kufuatia mgomo wa madaktari na wauguzi.

Madaktari na wauguzi wameanza mgomo wao hii leo, huku polisi wakitumia mabomu ya machozi kuwasambaratisha mamia ya madaktari walioandamana kushinikiza kulipwa malipo mazuri nje ya Wizara ya Afya Jijini Nairobi.

Madaktari hao waliovalia makoti yao meupe na kofia wanazovaa wakati wa upasuaji, walikuwa wameandamana kuishinikiza serikali kuheshimu makubaliano ya mwaka 2013 ya kuongezewa mishahara yao.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni