.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 4 Desemba 2016

WAZIRI MKUU AKABIDHI PIKIPIKI KWA VIJANA 200 JIJINI ARUSHA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema amekabidhi pikipiki 200 zenye thamani ya sh. milioni 400 kwa vijana 200 wa Jiji la Arusha, ili kuweza kuwakwamua kiuchumi vijana hao ambao walikuwa wakiendesha pikipiki za watu ambazo hazina tija.

Pikipiki hizo zimechangwa na wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani Arusha baada ya Mkuu wa Mkoa huo Bw. Mrisho Gambo kubuni mpango huo ambao umewawezesha vijana kupata pikipiki bila riba wala dhamana.

Waziri Mkuu alikabidhi pikipiki hizo jana jioni (Jumamosi, Desemba 3, 2016) mara baada ya kumaliza kuhutubia maelfu ya wananchi waliohudhutia katika mkutano wa hadhara kwenye uwanja cha Sheikh Amri Abeid.

Baada ya kukabidhi pikipiki hizo, Waziri Mkuu aliwataka vijana kuhakikisha wanakuwa waaminifu kwa kufanya kazi kwa bidii ili pikipiki ziweze kuwasaidia kuwainua kipato.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu alisema mwananchi yeyote hata kama si mtumishi wa umma anawajibu wa kuiheshimu Serikali na kuitumikia.Hivyo aliwataka vijana hao kuwa waadilifu.

“Serikali ya awamu ya tano imeanza kazi na moja kati ya majukumu yetu ni kuboresha nidhamu ndani na nje ya Serikali hivyo ni lazima ipate heshima yake,”.

“Tumeamua kuwatumikia. Tumeamua kuwahudumia watanzania wote bila ya kujali itikadi zao za kisiasa na kidini na Mheshimiwa Rais anataka kuona wananchi wake akifurahia Serikali yao,” alisema.

Kwa upande wake Bw, Gambo alisema pikipiki hizo zilizokabidhiwa kwa vijana hao zimetolewa sanjari na bima kubwa (Comprehensive Insurance) kwa vijana 200 ambapo kila Kata ilitoa vijana wanane.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu alisema zaidi ya sh. bilioni 800 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Arusha.

Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi alisema kati ya fedha hizo sh. bilioni 476 zitatumika katika ujenzi wa miradi wa maji ili kumaliza kero hiyo. 


“Mkoa wa Arusha unakabiliwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji safi na salama, hivyo fedha hizo zinalenga kumaliza tatizo hilo ambalo limechangiwa na uharibifu wa mazingira,” alisema.

Alisema kiasi kingine cha sh. bilioni 264 kilitolewa ili kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika mkoa huo. 


“Umeme Arusha hautakiwi kukatikakatika huu ni mji wa utalii. Tanesco imarisheni mtandao wa usambazaji,”.

IMETOLEWA NA: 

OFISI YA WAZIRI MKUU 
JUMAPILI, DESEMBA 4, 2016.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni