.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 1 Desemba 2016

WAZIRI MKUU AONGOZA MAMIA KUAGA MWILI WA MZEE XAVERY PINDA

jky1
Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete akizungumza wakati aliposhiriki katika kuaga mwili wa Marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
jky2
Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akizungumza wakati wa kuaga mwili wa marehemu baba yake, Xavery Mizengo Pinda kijijini kwake Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
jky3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakati aliposhiriki katika kuaga mwili wa baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu, marehemu Xavery Mizengo Pinda kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
jky4
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
jky6 jky7
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
jky8
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
jky9
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza wakati aliposhiriki katika kuaga mwili wa Marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
jky10 jky11
Baadhi ya waombolezaji walioshiriki katika kuaga mwili wa marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni Baba mzazi wa Waziri Mkuu, Mstaafu, Mizengo Pinda kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
jky12
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete wakiwa nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda kwenye kijiji cha Zuzu, Manispaa ya Dodoma ambako walishiriki katika kuaga mwili wa baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu, marehemu Xavery Mizengo Pinda Novemba 30, 2016. Wengine pichani kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
jky13


Waziri Mkuu, KassimMajaliwa akizungumza na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda baada ya kuaga mwili wa marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
jky14
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda baada ya kuaga mwili wa marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016.Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na wapili kulia ni Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
jky15
Waziri Mkuu, Mstaafu, Mizengo Pinda akipewa pole na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Alex Malasusa wakati awa kuaga mwili wa Baba yake mzazi wa Waziri Mkuu mstaafu, marehemu, Xavery Mizengo Pinda, kijijini Zuzu kwenye Manispa ya Dodoma Novemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
jky16
Baadhi ya waombolezaji walioshiriki katika kuaga mwili wa marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni Baba mzazi wa Waziri Mkuu, Mstaafu, Mizengo Pinda kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
jky17
Baadhi ya waombolezaji walioshiriki katika kuaga mwili wa marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni Baba mzazi wa Waziri Mkuu, Mstaafu, Mizengo Pinda kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
jky18
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo baada ya kuwasili nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda kushiriki katika kuaga mwili wa Baba mzazi wa Waziri Mkuu, Mstaafu Marehemu, Xavery Mizengo Pinda kwenye kijiji cha Zuzu, Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
jky19
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,Christina Mndeme na viongozi wengine wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa marehemu Mzee Xavery Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Pinda.

Mzee Xavery alifariki dunia Novemba 27, 2016 saa 9.30 alasiri katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Akizungumza wakati wa kuaga mwili huo nyumbani kwa Mheshimiwa Pinda kijijini Zuzu, Manispaa ya Dodoma leo (Jumatano, Novemba 30, 2016) Waziri Mkuu ametoa pole kwa wanafamilia na kuwaomba waendelee kumuombea marehemu apumzike mahala pema peponi.

Amesema msiba huo ni mzito, hivyo anawaomba wanafamilia wawe watulivu na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.

Wakati huo huo Waziri Mkuu amemuhakikishia Mheshimiwa Pinda kwamba Serikali iko pamoja naye katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mzazi wake.

“Serikali imetoa ndege kwa ajili ya kusafirisha msiba na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe ataiwakilisha Serikali katika mazishi hayo,” amesema.

Naye Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Kikwete amesema marehemu Mzee Xavery alikuwa mwema sana na alikuwa na upendo kwa watu wote.

“Baba yake Pinda alikuwa baba yangu pia. Alitambua ugumu wa kazi tulizokuwa tunazifanya na alitutaka tuwe wavumilivu,” amesema.

Kwa upande wake Mheshimiwa Pinda aliwashukuru viongozi wa Serikali, vyama vya siasa na wananchi kwa kutenga muda wao na kwenda kumfariji kufuatia msiba huo mzito. “Kuondokewa na baba mzazi au mwanafamilia yeyote si jambo dogo”.

Awali akisoma wasifu wa marehemu, Edward Kyungu ambaye ni mjukuu alisema Mzee Xavery alizaliwa mwaka 1926 katika kitongoji cha Mbede akiwa ni mtoto wa pekee wa Mzee Mizengo Pinda na Mama yake Wakalyate (Umartina).

Mzee Xavery alikuwa Katekista kazi ambayo aliifanya kuanzia mwaka 1951 hadi 1972 alipoamua kustaafu.

“Kazi ya pili ambayo alianza kuifanya kabla na hata wakati wa Ukatekista ni ukulima, jambo ambalo amewarithisha watoto wake wote na ndio maana wameachiwa sifa moja ya kuitwa watoto wa mkulima,” amesema.

Mzee Xavery anatarajiwa kuzikwa kesho (Alhamisi, Desemba Mosi, 2016) katika kijiji cha Kibaoni wilaya ya Mlele mkoani Katavi. Marehemu ameacha mke, watoto wanane, wajukuu 54 na vitukuu 40.
 

IMETOLEWA NA: 
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
S. L. P. 980, DODOMA.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni