.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 2 Desemba 2016

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO AFUNGUA KITUO CHA TAALUMA YA UHASIBU (NBAA) BUNJU

mawe-8
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt Philip Mpango (Mb), akihutubia baada ya kufunguliwa rasmi kwa Kituo cha Taaluma ya Wahasibu (APC) kilichojengwa na Bodi ya taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu katika eneo la Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam, ambacho ujenzi wake umegharimu shilingi Bilioni 33.
mawe-10
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt Philip Mpango (Mb), akimkabidhi Tuzo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Prof. Isaya Jairo, ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake katika kufanikisha ujenzi wa Kituo cha Taaluma ya Wahasibu (APC) kilichojengwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), katika eneo la Bunju nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam na kugharimu shilingi Bilioni 33.
mawe-4
Waziri wa Fedha na Mipango. Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC) cha Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwaniaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, katika eneo la Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam.
mawe-5
Baadhi ya wadau walioshuhudia Waziri wa Fedha na Mipango. Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akifungua rasmi Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC) cha Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwaniaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, katika eneo la Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam. Kituo hicho kimegharimu shilingi Bilioni 33.
mawe
Sehemu ya Majengo ya Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (Accountancy Profession Center-APC) cha Bodi ya Uhasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kilichofunguliwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, katika eneo la Bunju, Nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam
mawe-1
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akiwasili katika viunga vya kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC) cha Bodi ya Uhasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) katika aneo la Bunju nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam na kulakiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA Prof. Isaya Jairo (Katikati) na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni wa watumishi wa Serikali-GEPF, Bi. Joyce Shaidi
mawe-2
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akisalimiana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Musa Juma Assad, kabla ya kuzindua Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC) cha Bodi ya Uhasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, katika eneo la Bunju nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam.
mawe-3
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (wa tatu kutoka kulia) akiambatana na wakandarasi waliojenga Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC) pamoja na wajumbe wa Bodi na Uongozi wa NBAA, kukagua baadhi ya miundombinu ya kisasa iliyopo katika kituo hicho kilichopo katika eneo la Bunju, Nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam.
mawe-6
Meza Kuu wakiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (wa nne kutoka kulia) wakiimba Wimbo wa Taifa kabla ya kuanza hotuba mbalimbali, baada ya kufunguliwa rasmi kwa Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC) cha Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kilichojengwa eneo la Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam.
mawe-7
Wasanii, Mrisho Mpoto na Banana Zoro, wakitumbuiza wakati wa tukio la kufunguliwa rasmi kwa Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC) cha Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kilichojengwa eneo la Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam.
mawe-9
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt Philip Mpango (Mb), akihutubia baada ya kufungua rasmi kwaniaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Kituo cha Taaluma ya Wahasibu (APC) kilichojengwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu katika eneo la Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam, kilichogharimu shilingi Bilioni 33.
mawe-11
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt Philip Mpango (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi (NBAA) baada ya kuhitimishwa kwa tukio la kufunguliwa rasmi kwa Kituo cha Taaluma ya Wahasibu (APC) kilichojengwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), katika eneo la Bunju nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam na kugharimu shilingi Bilioni 33.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni