.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 4 Januari 2017

ARSENAL YAPONEA KWENYE TUNDU LA SINDANO MBELE YA BOURNEMOUTH

Timu ya Arsenal imepambana kiume na kuchomoa magoli matatu waliyofungwa katika dakika za majeruhi na Bournemouth na kulazimisha sare ya magoli 3-3.

Arsenal ilionekana kama inapata kipigo cha tatu ugenini, ilianza kuchomoa magoli hayo kwa kichwa cha kuchupa cha Alexis Sanchez na kisha Lucas Perez kutupia la pili na kufanya matokeo kuwa 3-2.

Bournemouth ilijikuta ikibakia na wachezaji 10 baada ya Simon Francis kutolewa nje kwa kumchezea rafu Aaron Ramsey na Arsenal kutumia upungufu huo kusawazisha kupitia kwa Olivier Giroud.
                                         Charlie Daniels akifunga goli la kwanza katika mchezo huo
 Olivier Giroud akiwa ameupiga kichwa mpira uliojaa wavuni na kuipa sare Arsenal

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni