Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Banadari Zanzibar Nd.Abdulla Juma kati katikakimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wa kwanza Kulia tatizo la eneo la bandari la Kigomasha ambalo kitaalamu haliwezi kujengwa Gati kutokana na kina kidogo cha maji yake ya Bahari. Wa kwanza kutoka Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mheshimiwa Omar Khamis Othman.

Balozi Seif akikagua Kitalu cha miche mbali mbaliya matunda, Viungo na Mbao kinachoendeshwa na Wananchi wa Kijiji cha Junguni ndani ya Mkoa Kaskazini Pemba chini ya Mradi wa Tasaf.

Balozi Seif akiridhika na hatua kubwa iliyofikiwana Wananchi wa Kijiji cha Junguni kwa ujenzi wa Jengo jipya la Skuli ya Maandalizi ya Kijiji hicho chini ya Mradi wa Maendeleo ya Jamii Tanzania {TASAF }. Picha na – OMPR – ZNZ.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameuagiza Uongozi wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji kuandaa mchakato wa kuwakutanisha Wataalamu wa Sekta hiyo ili wajadili na hatimae kupata kauli moja itakaobaini eneo muwafaka linalostahiki kujengwa Gati Rasmi ndani ya Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Alisema hatua hiyo inastahiki kutekelezwa vyema kama ilivyoagizwa na Serikali Kuu la kutaka kujengwa kwa Gati katika Bandari ya Kigomasha ili kujaribu kudhibiti mapato ya Taifa yanayotokana na uingiaji na utokaji holela wa vyombo vya Baharini pamoja na usalama wa eneo hilo.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa agizo hilo alipokagua Bandari ya Kigomasha ambayo baadhi ya Wavuvi huitumia kusafirishia magendo akiwa katika ziara ya Siku Tatu Kisiwani Pemba kuangalia miradi ya Maendeleo na ile ya Ustawi wa Jamii.
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeshaamua na kutoa mapendekezo ya kujengwa kwa Bandari Rasmi ndani ya Mkoa wa Kaskazini
Pemba.
Pemba.
Alisema Uongozi wa Jumuiya ya Uchumi ya Afrika Mashariki tayari umeshalipigia kelele eneo hilo la Bandari ya Kigomasha linaloonekana kutumiwa na watu wasiofahamika mazingira yao wakitokea nje ya Visiwa
vya Zanzibar jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa Taifa.
vya Zanzibar jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa Taifa.
Balozi Seif alieleza kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kutumia vyombo vyake vya ulinzi lazima itengeneze mazingira kuvihami Visiwa vyake kutokana na dalili zilizo wazi zinazobainisha baadhi ya wahalifu wanaingia Nchini kinyume na taratibu zilizowekwa za Uhamiaji.
Mapema Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Nd. Abdulla Juma
alisema eneo la Kigomasha limekuwa na kina kidogo cha maji kiasi kwamba Kitaalamu inakuwa vugumu kulitumia kwa shughuli za Bandari licha ya kupendekezwa na Idara ya Uhamiaji kutokana na uingiaji holela wa wageni.

Nd. Abdulla alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba lipo
eneo Shumba Mjini ndani ya Mkoa wa Kaskazini Pemba ambalo linaweza
kutumiwa kwa shughuli za Gati endapo litawekewa mazingira mazuri ya
Miundombinu kutokana na kina kikubwa cha maji.
eneo Shumba Mjini ndani ya Mkoa wa Kaskazini Pemba ambalo linaweza
kutumiwa kwa shughuli za Gati endapo litawekewa mazingira mazuri ya
Miundombinu kutokana na kina kikubwa cha maji.
Naye kwa upande wake Kamanda wa Idara ya Uhamiaji Kisiwani Pemba Abdi
Bulushi Juma alisema Kigomasha ni eneo sugu linaloleta usumbufu kwa askari wake wakati wanapofanya doria.
Bulushi Juma alisema Kigomasha ni eneo sugu linaloleta usumbufu kwa askari wake wakati wanapofanya doria.
Alisema bandari Bubu ya Kigomasha imekuwa kero na ikiripotiwa matukio
mengi ya uingiaji na usafiri wa watu wasiozingatia taratibu zilizowekwa za uhamiaji sambamba na shughuli za magendo ya Karafuu.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
mengi ya uingiaji na usafiri wa watu wasiozingatia taratibu zilizowekwa za uhamiaji sambamba na shughuli za magendo ya Karafuu.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni