Bondia Iddi Mkwela kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Vicent Mbilinyi wakati wa mazoezi yake wa kujiandaa na kupigana na Manyi Issa Feb 5 katika uwanja wa ndani wa Taifa 'Indoor Stadium' mpambano wa raundi kumi uzito wa KG 61 Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Bondia Iddi Mkwela akielekezwa kupiga ngumi zenye mkunjo wa chini 'Upcat' na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' wakati wa mazoezi yanayoendelea katika Super D gym iliyopo kariakoo shule ya uhuru Mkwela atazipiga na Manyi Issa Feb 5 katika uwanja wa ndani wa Taifa 'Indoor Stadium' mpambano wa raundi kumi uzito wa KG 61 Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Iddi Mkwela akielekezwa kupiga ngumi zilizo nyooka na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' wakati wa mazoezi yanayoendelea katika Super D gym iliyopo kariakoo shule ya uhuru Mkwela atazipiga na Manyi Issa Feb 5 katika uwanja wa ndani wa Taifa 'Indoor Stadium' mpambano wa raundi kumi uzito wa KG 61 Picha na SUPER D BOXING NEWSNa Mwandishi Wetu
BONDIA Iddi Mkwela ameingia kambini baada ya kusaini mpambano wake wa raundi kumi uzito wa kg 61 kupambana na Manyi Issa Feb 5 katika uwanja wa ndani wa Taifa
Mpambano uho wa mabondia hawo unatarajia kuwa mzuri sana kwa kuwa mabondia wote ndio kwanza wananza kuwika katika tasinia ya masumbwi na ndio mpambano uliobeba hisia za wapenzi na mashabiki wengi wa mchezo wa ngumi kutokana na kutajwa mara kwa mara kwa wapenzi wa wanaofatilia mchezo wa ngumi kwa sasa nchini
Akizungumza kuhusu mpambano wake uho Mkwela amesema kuwa anae mtafuta sio yeye kabisa kwani ayupo katika akili yangu kwa kuwa kesha jipendekeza huyu atakuwa kafanywa kafala kwani ndio njia yangu ya kwenda kwa mabondia ninao wataka huyu sio saidi yangu ngumi ajajua ili mikono ita ongea siku hiyo sina maneno mengi alisema Mkwela;
Nae kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' anae mnowa bondia huyo amesema kwa kuwa mpambano wa kwanza kwa Mkwela kucheza raundi kumi naitaji nimwangalie pumzi yake kwani mazoezi anafanya mengi ya nguvu na ana bidii ya mazoezi matumaini yangu atashinda ushindi ambao ato wasumbua majaji kuandika katika karatasi zao yani K.O ya mapema
Ahidha siku hiyo kutakuwa na mapambano mbalimbali ya kukata na shoka ambapo bondia kutoka mbeya Meshack Mwankemwa atakumbana na Ramadhani Shauri katika mpambano wa raundi kumi za ubingwa
Mpambano mwingine utawakutanisha bondia Mohamed Matumla atakaevaana na Mfaume Mfaume wengine ni Mohamed Swedi atakae vaana na Ahidar Mchenjo na Ibrahimu Maokola atazipiga na Zumba Kukwe kutoka Kibaha pamoja na mapambano mengine mbalimbali
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni