Kocha wa Leicester City, Claudio
Ranieri, ametajwa kuwa kocha wa mwaka katika hafla ya utoaji tuzo za
Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) katika hafla iliyofanyika Jijini
Zurich.
Muitaliano huyo alikuwa akichuana na
kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane na kocha wa Ureno Fernando
Santos kuwania tuzo hiyo.
Ranieri aliiongoza timu ya Leicester
kuweka historia ya kutwaa kombe la Ligi Kuu ya Uingereza 2016, ambayo
msimu wa mwaka 2015 ilinusurika kushuka daraja.
Diego Maradona akimpa tuzo kocha Claudio Ranieri
Kocha mwanamke Mjerumani Slivia Neid naye alitwaa tuzo ya Fifa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni