Shirikisho la Soka Duniani (FIFA)
limeamua kuongeza timu za taifa zitakazo shiriki michuano ya Kombe la
Dunia na kuwa timu 48, kutoka timu 32 za sasa.
Katika hatua ya awali makundi 16 ya
timu tatu yatacheza mechi za mitoano ili kubakia na timu za taifa 32,
ikiwa ni mabadiliko yaliyofanywa kwa michuano ya kombe la dunia ya
mwaka 2026.
Shirikisho la Soka la Fifa, limepiga
kura nyingi za kuridhia mabadiliko hayo katika mkutano wao
uliofanyika hii leo Jijini Zurich.
Kwa mabadiliko hayo mechi za
michuano hiyo zitaongezeka na kuwa 80, kutoka 64 za sasa hata hivyo
bado washindi watacheza mechi saba.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni