Wafungwa wapatao 33 wameuwawa katika
gereza kaskazini mwa Brazil, ikiwa ni siku chache tu kupita tangu
wafungwa 56 kufa wakati wa ghasi zilizotokea kwenye gereza la jimbo
jirani.
Miili 30 imekutwa ikiwa
imetenganishwa vichwa vyao na viwiliwili maafisa wa gereza hilo la
Brazili wamesema.
Waziri wa Sheria wa jimbo hilo Uziel
Castro amelishutumu kundi la dawa za kulevya la Roraima kwa kuhusika na mauaji hayo.
Hata hivyo hali katika gereza hilo
la Monte Cristo lenye mrundikano wa wafungwa imerejea katika hali ya
utulivu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni