.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 16 Januari 2017

IBADA ZA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA.

Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Soko Kuu la Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, wakifuatilia mahubiri na mafundisho ya neno la Mungu kutoka kwa Mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola, kwenye ibada za jana jumapili, Januari 15,2017.

Kulikuwa na somo zuri liitwalo “KWELI MUNGU YUPO” kutoka kitabu cha 1-Wafalme 18 hivyo soma kwa kitabu hicho ili ujifunze zaidi kuhusiana na uwepo wa Mungu ukimtafuta kwa uaminifu.
Watoto wakimsikiliza kwa makini Mchungaji, Dkt.Daniel Moses Kulola, baada ya kuwaombea ili kuelekea kwenye mafundisho yao
Jumapili ibada ya kwanza huanza saa 12:00 asubuhi, ibada ya pili saa 01:00 asubuhi na ibada ya tatu saa 04:30 asubuhi huku ibada za katikati ya juma zikifanyika jumatano na ijumaa kuanzia saa 10:00 alasiri.
Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza, akiwemo mama Mchungaji Mercy Daniel Kulola (katikati), wakiwa kwenye maombi kanisani hapo
Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza, wakifuatilia ibada kanisani hapo
                                         Hakikisha hukosi ibada za Kanisa la EAGT Lumala Mpya.
                                          Picha na Craty Christopher @EAGT Lumala Mpya Church

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni