James Rodriguez amefunga magoli
mawili wakati Real Madrid ikiweka rekodi ya kucheza michezo 38 bila
ya kufungwa, na kuibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Sevilla
katika michuano ya kombe la Copa del Rey.
Rodriguez alipewa nafasi ya kucheza
mzunguko wa kwanza wa kombe hilo, wakati huu gareth Bale akipona
majeruhi na Cristiano Ronaldo akiwa amepumzishwa, ambapo aliyafunga
magoli hayo yote katika kipindi cha kwanza.
Rodriguez alikuwa wa kwanza kufunga
goli katika dakika ya 11 na baadaye Raphael Varane kuongeza la pili
katika dakika ya 29, na kisha Rodriguez akafunga goli la tatu kwa
mkwaju wa penati.
Raphael Varane akishangilia baada ya kufunga goli la pili
James Rodriguez akiwajibiga uwanjani kuwania mpira na Mariano Ferreira
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni