Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Zanzibar Bw. Joseph Meza (wa kwanza kulia) akiongoza kikao kazi cha Makatibu Wakuu kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katikati ni Mwenyekiti Mwenza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Muungano kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Dar es Salaam Bw. Baraka Rajab. Kikao kazi hicho kimefanyika leo tarehe 05/01/2017 katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na kwa pamoja wamejadili changamoto za Muungano.
Baadhi ya Makatibu Wakuu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia kikao kazi kilichojadili changamoto za Muungano. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Baadhi ya Makatibu Wakuu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia kikao kazi kilichojadili changamoto za Muungano. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Bw. Shomari Omar Shomari Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Bi. Fatma Gharib Bilal Katibu Mkuu Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto na Bi. Khadija Bakari Juma Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya amali kwa pamoja wakifuatilia kikao kazi kilichojadili changamoto za Muungano na namna bora ya kuzipatia ufumbuzi.
Mwenyekiti na Mwenyekiti Mwenza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Zanzibar Bw. Joseph Meza (wa pili kulia) na Prof. Faustin Kamuzora (wa tatu kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya kumalizika kwa kikao kazi.
Pichani ni Mwenyekiti na Mwenyekiti Mwenza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Zanzibar Bw. Joseph Meza (wa pili kulia) na Prof. Faustin Kamuzora (wa tatu kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti iliyoratibu kikao hicho ikiwa na wajumbe kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni