Mchezo wa kwanza wa kocha Pep
Guardiola wa FA umemalizikia kwa ushindi mnono baada ya Manchester
City kuichakaza West Ham kwa magoli 5-0 katika mchezo wa raundi ya
tatu.
Manchester City ilikuwa inaongoza
kwa magoli 3-0 hadi mapumziko ambapo Yaya Toure alifungua mvua ya
magoli kwa shuti la mpira wa penati.
Havard Nordtveit alitumbukiza
kimakosa mpira kwenye wavu wao kufuatia krosi ya Bacary Sagna, katika
sekunde ya 146 kabla ya David Silva kufunga la tatu.
Muda mfupi baada ya kuanza kipindi
cha pili Sergio Aguero aliunganisha wavuni mpira uliopigwa na Toure
na kisha John Stones kufunga la tano.
Mpira wa penati uliopigwa na Yaya Toure ukijaa wavuni
Sergio Aguero akiangalia mpira alioupiga kwa kuudokoa ukielekea wavuni
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni