.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 16 Januari 2017

MAJALIWA AZINDUA SAFARI ZA NDEGE ZA ATCL KATI YA DAR NA DODOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea mfano wa Boarding Pass kutoka kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mahandisi Edwin Ngonyani kabla ya kusafiri kwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kutoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere, Dar es salaam kwenda Dodoma Januari 16, 2017. Alikuwa akizindua safari za ndege za shirika hilo kati ya viwanja viwili hivyo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisafiri kwa ndege ya Bombardier Q400 ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kutoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere kwenda Dodoma Januari 16, 2017. Alikuwa akizindua safari za ndege za ATCL katika viwanja viwili hivyo. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Leonard Chamuriho. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia viongozi na wananchi wa Dodoma baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Januari 16, 2017 ikiwa ni uzinduzi wa Safari za ndege za Shirika hilo kati ya viwanja viwili hivi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Januari 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana ​ baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kati ya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2016. Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijan, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Kapteni Richard Shaidi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ATCL kati ya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2017. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Leonard Chamuriho. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Christina Mndeme. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kabla ya kupanda ndege ya Shirika hilo kwenye uwanja wa Ngege wa Julius Kambarage Nyerere kwenda Dodoma ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati ya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Ngege ya Tanzania (ATCL) baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati aya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati aya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Spika wa Bunge, Job Ndugai baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati aya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Kapteni Richard Shaidi akizungumza katika uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati ya Uwnja wa Julius Kambarage Nyerere na Dodoma,mjini Dodoma Januari 16, 2017. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana akizungumza katika uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati ya Uwnja wa Julius Kambarage Nyerere na Dodoma,mjini Dodoma Januari 16, 2017. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, akizungumza katika uzinduzi wa safari za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kati ya uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere na Dodoma Januari 16, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mstaafu John Malecela akizungumza katika uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati ya Uwnja wa Julius Kambarage Nyerere na Dodoma,mjini Dodoma Januari 16, 2017. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua safari za ndege za Shirika la Ndege la Tanzania kati ya uwanja wa Julius Kambarage Nyerere na Dodoma katika hafla iliyofanyika kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Januari 16, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni