Son Heung-min amefunga goli katika
dakika za mwisho na kuisaidia Tottenham kuibuka na ushindi, ikitokea
kuwa nyuma goli moja dhidi ya timu ya daraja la pili ya Wycombe
katika mchezo wa kombe la FA,
Mchezaji Paul Hayes, ambaye awali
mpira uligonga mwamba aliishtua timu ya Ligi Kuu ya Uingereza kwa
goli la shuti la mguu wa kushoto na kuifanya Wycombe iongoze kwa goli
moja.
Kapteni huyo wa Wycombe alifunga
goli la pili kwa mwaju wa penati, hata hivyo goli la Son na la penati
lililofungwa na Vincent Janssen na matokeo kuwa 2-2.
Garry Thomson aliyetokea benchi
alifunga kwa kicha mpira wa krosi ya Myles Weston na kuifanya
Waycombe iongoze tena lakini Dele Alli alisawazisha na Son kufunga
goli la nne la ushindi.
Garry Thomson akifunga goli baada ya kutokea benchi katika mchezo huo
Son Heung-min akifunga goli la ushindi la Tottenham katika dakika ya 90+7



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni