Mwanamuziki Adele ameonekana kukataa
ushindi wake wa tuzo ya Grammy ya albamu bora, na kusema mwanamuziki
Beyonce ndiye anayestahili kupata tuzo hiyo.
Msanii huyo wa muziki aliyetwaa tuzo
tano za Grammy, aliwaambia watu waliofika katika hafla ya utoaji wa
tuzo hizo, kuwa hawezi kuikubali tuzo hiyo.
Ushindi wa Adele dhidi ya Beyonce ni
dhahiri unachochea malalamiko kuwa tuzo za Grammy huwa zinawabania
wasanii weusi.
Beyonce akiwa na mumewe Jay-Z wakimsikiliza Adele kwa hisia kali
Beyonce akitiririkwa na machozi kutokana kuguswa na maneno aliyotoa Adele
Mwanamuziki Adele akiwa amepozi na tuzo zake tano za Grammy alizozitwaa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni