.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 27 Februari 2017

BALOZI SEIF AONYA WANAOENEZA UVUMI KUPITIA MITANDAO

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif
Ali Idi amewaasa wana CCM na wananchi wote Nchini kuacha tabia ya
kuhamanika kutokana na uvumi unaoenezwa mitandaoni kwamba yapo
mabadiliko ya utawala wa Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika hivi
karibuni.
 

Alisema Wananchi wanapaswa kuelewa kwamba uchaguzi Mkuu wa Zanzibar
umekwisha kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 na kuwataka
kuelekeza nguvu zao katika kusimamia mirai yao ya maendeleo.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa nasaha hizo wakati akitoa salamu kwenye
Hafla ya ugawaji wa vifaa vya michezo kwa Timu za Soka zitakazoshiriki
mashindano ya Ligi ya Majimbo hapo ukumbi wa CCM Mkoa Amani Mjini
Zanzibar ambapo Mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed
Shein.

Aliwatanabahisha wale wote wanaoendeleza kasumba ndani ya mitandao ya
Kijamii kwa kuwadanganya Wananchi kwa makusudi waendelee kuvumilia na
kustahamili hadi utakapofika uchaguzi mwengine Mkuu wa Mwaka 2020.

Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
aliwahakikishia Wazanzibari na Watanzania wote kwa jumla kwamba Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein
ataendelea kuviongoza Visiwa vya Unguja na Pemba hadi utakapofanyika
uchaguzi mwengine mwaka 2020 kama Katiba ya Zanzibar inavyoeleza.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
26/2/2017.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni