Barcelona imeifunga Atletico Madrid
katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Copa del Rey katika dimba
la Vicente Calderon.
Katika mchezo huo ulioishia kwa
magoli 2-1, Luis Suarez aliwafanya vinara waongoze kwa goli
alilofunga kwa kutoka umbali wa nusu ya kiwanja na kumalizia
kiufundi.
Lionel Messi aliongeza goli la pili
la Barcelona, lakini Antoine Griezmann, akaipatia Atletico matumaini
katika mchezo wa marudiano jumanne wiki ijayo katika dimba la Nou
Camp.
Lionel Messi akishangilia baada ya kufunga goli la pili
Antoine Griezmann akifunga goli kwa mpira wa kichwa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni