David Beckham ameonyesha ujuzi wake
wa kupika chapati za maji, katika Siku ya Chapati ya Maji kwa
kuonyesha majonjo ya kugeuza chapati.
Mchezaji huyo wa zamani wa
Manchester United, anaonekana akizungusha chapati aliyokuwa akipika
kikaangoni na kisha kuigeuza kwa kuirusha juu.
Katika video yake aliyotupia kwenye
Instagram Beckham anasikika akiwatakia watoto wake siku njema ya
chapati, huku akifurahia namna alivyogeuza chapati aliyopika.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni