Dubai, UAE; Tarehe 02 Februari 201 / --
- Imeripoti faida ya jumla ya mwaka mzima ya AED milioni 31.6 (USD milioni 8.6)
- Mapato ya jumla ya mwaka yamefika AED bilioni 5 (USD bilioni 1.37) kwa kipindi cha miezi 12
- Imebeba idadi kubwa zaidi ya abiria (milioni 10.4) na kushuhudia ukuaji wa 14.4% ikilinganishwa na mwaka uliopita
flydubai (www.flydubai.com) leo imetangaza matokeo yake ya mwaka mzima wa 2016, huku ikiripoti faida ya AED milioni 31.6 (USD milioni 8.6). Imetangaza mapato ya jumla ya AED bilioni 5 (USD bilioni 1.37), ambalo ni ongezeko la 2.4% ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita. Matokeo bora ya nusu ya pili ya mwaka, yaliyotokana na ongezeko la idadi ya abiria, yaliathiriwa na kupunguka kwa abiria, hivyo basi kusababisha viwango vya chini vya ukuaji wa mapato ya jumla. Hali hii inaashiria kuendelea kuwepo kwa sababu zile zile ambazo ziliripotiwa kuathiri mapato ya nusu ya kwanza ya mwaka.
Mheshimiwa Sheikh Ahmed bin Saeed Al Maktoum, Mwenyekiti wa flydubai, alisema: “matokeo haya yamewezesha flydubai kuripoti faida ya mwaka mzima kwa mwaka wa tano mfululizo. Mwaka 2012, ambao ulikuwa mwaka wetu wa tatu wa kutoa huduma, tulisafirisha abiria milioni 5.1. Mwaka huu, tumesafirisha abiria milioni 10.4, kuonyesha kwamba flydubai inaendelea kusaidia kuboresha safari za biashara na burudani katika eneo hili lote. Hitaji la kuongezeka kwa muunganisho wa kiusafiri umewezeshwa na sifa za kitalii za UAE na ukweli kwamba eneo hili ni kitovu cha kimataifa cha biashara, pamoja na ubora wa kijiografia za UAE.”
Ghaith Al Ghaith, Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa flydubai, akirejea Matokeo ya Mwaka wa 2016, alidokeza: “Katika miaka miwili iliyopita, tumeshuhudia ongezeko la 52% la idadi ya abiria kwa msingi wa RPKM [1]. Tunaendelea kuthibitisha kwamba tunapata wateja waaminifu katika mtandao wetu wote, ambao wanatambua manufaa ya safari zetu za ndege za moja kwa moja na kufurahia huduma zetu za safari za ndege. Kuendelea kwa mapunguzo ya bei za mafuta na juhudi endelevu za kudhibiti gharama, zimechangia katika ukuaji wa 16% kwa msingi wa ASKM [2] katika miaka miwili iliyopita. Hata hivyo, tumeshuhudia mazingira magumu ya bei na utendaji.”
Utendaji wa gharama na mapato
EBITDAR [3] ilikuwa bora katika mapato kwa 21.1%; hili ni ongezeko ikilinganishwa na mwaka uliopita, ambapo yalikuwa 20.5%.
Nafasi ya kufunga ya fedha na rasilmali, ikiwa ni pamoja na malipo ya kabla ya kuwasilishwa kwa bidhaa za baada za malipo kwa ajili ya ndege za baadaye, zilibakia imara katika thamani ya AED bilioni 2.3.
Gharama za mafuta zilikuwa 25% ya gharama za uendeshaji wa huduma, ikilinganishwa na 30.6% mwaka uliopita, kufuatia mapunguzo ya bei ya mafuta mwaka huu, na amana ya utabiri wa bei ya mafuta iliathiri 21% tu ya kiasi kamili mwaka wa 2016.
Visaidizi vya mapato, vinavyojumuisha mizigo, shehena na mauzo ya ndani ya ndege, vilichangia 13.8% ya mapato; na haya yalipungua ikilinganishwa na mwaka uliopita, ambapo yalikuwa 15.1%.
Uendeshaji wa huduma
Ununuzi wa ndege: Ndege 8 za Kizazi Kipya za Boeing 737-800 ziliongezwa katika mwaka wa 2016 katika juhudi za kuongeza huduma za usafiri. Ndege zote zilikuwa zimetumika kwa takribani miaka 3 na miezi 8.5.
Daraja la Biashara: Daraja la biashara: ongezeko la idadi ya abiria wa Daraja la Biashara wa flydubai uliendelea na kushuhudia kampuni kubeba abiria zaidi mara 2.4 zaidi kuliko mwaka wa 2014. Eneo hili la bara lilishuhudia mahitaji ya juu zaidi ya abiria wa Daraja la Biashara ambao walikuwa mara mbili zaidi ya idadi kawaida ya wasafiri. Hili lilifuatiwa na Caucasus, ambayo ilikua kwa 88%, kufuatia ulegezaji wa masharti ya sheria za viza, hivyo kusababisha ongezeko la mahitaji kutokana na safari za kuingia na kuondoka kwa abiria. Aidha, abiria wa Daraja la Biashara waliongezeka kwa 38% katika Ulaya na 24% katika GCC na Mashariki ya Kati.
Upanuzi wa huduma: Katika kipindi cha mwaka huu, kulikuwa na ongezeko la safari za ndege kwenye njia zilizopo pamoja na kuimarika kwa utendaji wa njia 41 mpya zilizoanzishwa mwaka wa 2014 na 2015 kulisababisha ukuaji wa ASKM kwa 9%.
Uzinduzi huu wa tarehe 29 Novemba wa safari za ndege za mji maarufu wa Bangkok, ilikuwa njia ya kwanza ya nje ya GCC, kuanza utendakazi kwa huduma zilizoongezeka kuwa mara mbili kila siku. Katika sehemu zote, flydubai iliripoti idadi ya abiria ifuatavyo:
- GCC na Mashariki ya Kati: flydubai ilibebea 28% ya abiria wote kati ya Dubai na GCC na Mashariki ya Kati.
- Ulaya: idadi ya abiria barani Ulaya iliongezeka kwa 19%.
- Urusi: idadi iliongezeka kwa 3% kufuatia safari 21 za ndege kila wiki kwenda miji 7.
- Ukraini: idadi jumla ya abiria wa flydubai waliosafiri kati ya Ukraini na Dubai iliongezeka kwa 26%.
- Asia ya Kati (Kazakistani, Kirgizia, Tajikistani na Tukmenistani): maeneo yake 5 katika eneo hili yalishuhudia flydubai ikichangia 23% ya ukuaji wa jumla katika viwanja vya ndege vya Dubai.
- Eneo hili la bara: idadi ya abiria kwenye mtandao wa flydubai iliongezeka kwa 22%.
- Afrika: idadi ya abiria katika maeneo yake 11 iliongezeka kwa 3% na kuchangia ongezeko la jumla la 12% katika viwanja vya ndege vya Dubai.
Al Maktoum Kimataifa (DWC): flydubai imekuwa ikihudumu kutoka DWC tangu Oktoba 2015. Kufuatia viingilio vyake viwili vya eneo, flydubai itaendelea kuongeza huduma zake katika DWC polepole kulingana na upanuzi zaidi wa uwanja huu wa ndege.
Idadi ya wafanyakazi: flydubai iliendelea kukuza timu yake ya wahudumu wenye uzoefu hadi jumla ya wafanyakazi 3,773, ikiwa ni pamoja na marubani 746, wahudumu wa abiria 1,618 na wahandisi 282.
HALI YA WAZI: flydubai ilianzisha mpango wake wa zawadi, ambao ni rahisi na wa moja kwa moja, tarehe 25 Oktoba 2016, na umepokelewa vizuri katika soko.
Takwimu Kuu za Uendeshaji Huduma
Tarehe 31 Desemba 2016
|
Tarehe 31 Desemba 2015
|
Asilimia(%) ya
Ongezeko
| |
ASKM (milioni)
|
25,995
|
23,857
|
9.0
|
Idadi ya abiria (milioni)
|
10.4
|
9.04
|
14.4
|
Wingi wa ndege (Idadi ya ndege)
|
57
|
50
|
14.0
|
Mchango kwa jumla ya ukuaji katika viwanja vya ndege vya Dubai (asilimia)
|
21
|
11.5
|
haitumiki
|
Matumizi ya Ndege – wastani wa vipindi vya saa kwa kila ndege kila siku
|
13.5
|
13.6
|
haitumiki
|
Abiria wanaoondoka
|
88,114
|
81,530
|
8.1
|
FZ981: kufuatia ajali ya FZ981 tarehe 19 Machi 2016, flydubai bado inaendelea kusaidia familia waliopoteza wapendwa wao. Pamoja na kutoa malipo ya usaidizi wa kifedha wa awali na malipo ya usaidizi wa kifedha wa mpito, Timu Yetu ya Utunzaji wa Muda Mrefu inaendelea kuhudumia familia waliofiwa, ambao tunajali sana. Mipango ya kumbukumbu inaendelea kutayarishwa ili kuadhimisha mwaka wa kwanza tangu ajali hiyo kufanyika.
Ghaith Al Ghaith, Mkurugenzi Mtendaji wa flydubai, alisema: “flydubai, kupitia mwakilishi wake aliyeidhinishwa, inaendelea kusaidia katika uchunguzi wa ajali hiyo ya kusikitisha. Timu Yetu ya Usaidizi wa Muda Mrefu wa Familia, inaendelea kuhudumia familia zote.”
Matarajio
Mwaka huu wa 2017, flydubai itakuwa kampuni ya ndege ya kwanza katika Mashariki ya Kati kupokea muundo mpya wa Boeing 737 MAX 8, na ndege ya kwanza kati ya hizi itaanza kuhudumu katika nusu ya pili ya mwaka. Uwezo wa jumla hautaongezeka mwaka wa 2017, kwa sababu kuna mabadiliko katika mahitaji ya muda mfupi, kutokana na changamoto zinazoendelea katika mazingira ya uendeshaji wa huduma. Tangu kuzinduliwa, mojawapo ya kanuni za mikakati ya mipango ya ndege za flydubai imekuwa ni kudumisha ndege ambazo zimetumika kwa muda mfupi. Chini ya mipango hii, kampuni hii ya ndege itashuhudia mwisho wa kipindi cha kuhudumu kwa ndege 4 za Kizazi Kipya za Boeing 737 -800 na baadaye mwaka huu huduma za ndege hizi zitasitishwa.
Ghaith Al Ghaith, Mkurugenzi Mtendaji wa flydubai, akitazamia mwaka unaokuja, alisema: “tutakuwa makini mwaka wote wa 2017 kwa sababu tutaendelea kufanya kazi katika mazingira magumu ya kiuchumi. Tutajitahidi kupata faida na tunatarajia kupata ongezeko la kiwango sawa katika mwaka unaokuja. Tunatazamia kupokea ndege ya kwanza aina ya Boeing 737 MAX 8 katika eneo hili, ambayo itapunguza matumizi ya mafuta na kuleta ubora na ufanisi zaidi katika huduma zetu za ndege mpya. Tumejikita katika mkakati wetu wa kuongoza katika ubunifu, kutoa huduma za kipekee safarini na uwanjani, pindi tunavyoendelea kukidhi mahitaji ya usafiri wa abiria wetu.”
[1] Mwendo wa abiria wa mapato ya RPKM.
[2] Mwendo kulingana na viti vinavyopatikakana wa ASKM.
[3] EBITDAR huhesabiwa kama mapato kabla ya kuondoa gharama ya riba, kodi, uchakavu, madeni na kukodisha.
Kusambazwa na APO kwa niaba ya flydubai.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni