Maandalizi ya mchezo wa kesho wa kimataifa kati ya Young Africans ya Tanzania na Ng’aya ya Comoro, yamekamilika kwa asilimia 100.
Timu zote zipo Dar es Salaam, ambako Young Africans wao wameweka kambi kwenye Hoteli ya Zimbo iliyoko Kariakoo kwenye makutano ya mitaa ya Ndovu na Nyamwezi, Dar es Salaam.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
http://tff.or.tz/news/792-kuelekea-mchezo-wa-kesho-kati-ya-young-africans-n-gaya-club
MSIBA WA IKONGO JULIUS MBAGA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikito taarifa ya kifo cha Nahodha wa timu ya 94 Green Warriors, Ikongo Julius Mbaga aliyefariki dunia leo alfajiri (Februari 17, 2017) kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo alikuwa amelazwa.
Mchezaji huyo alijeruhiwa kwenye ajali ya gari ya timu yake iliyotokea Februari 13, 2017 Ihumwa mkoani Dodoma wakati ikiwa njiani kwenda Shinyanga kucheza mechi ya Ligi Daraja la Pili (SDL) dhidi ya Bulyanhulu FC.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
http://tff.or.tz/news/791-msiba-wa-ikongo-julius-mbaga
MSIBA WA GEOFFREY BONNY
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetuma salamu za rambirambi kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya kutokana na kifo cha mchezaji wa zamani Tanzania Prisons, Young Africans na timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
Taarifa kutoka Mbeya, zilizothibitishwa na uongozi wa Mkoa zinasema kwamba mchezaji huyo alifariki dunia usiku wa kuamkia leo Ijumaa Februari 17, 2017 kwenye Hospitali ya Wilaya ya Rungwe.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
http://tff.or.tz/news/790-msiba-wa-geoffrey-bonny

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni