.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 28 Februari 2017

MTOTO LATIFA ALIYEIBWA SAA MBILI ASUBUHI IRINGA MJINI APATIKANA USIKU KIJIJI CHA MKUNGUGU

Mtoto Latifa akiwa ambebwa na Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela walipofika kituo cha polisi.

Leo mida ya saa mbili asubuhi katika maeneo ya Stand kuu ya mabasi ya Iringa aliibiwa mtoto mchanga mweney umri wa miezi 5. Mtoto huyo inasadikwia aliibwa na binti ambaye alikuwa amekuja kutafuta kazi.

Akieleza tukio hilo Mama yake Bi Asha Shaban Lauza alisema " nikiwa naosha vyombo binti huyu ambaye toka jana alikuwa anatafuta kazi alianza kumpa maziwa mtoto yaliyo kwenye chupa mpaka mtoto akamaliza. Baadae mtoto akajinyea basi bila wasiwasi nikampa shilingi elfu kumi ili akanunue pampasi duka la pili tu akanyanyuka na mtoto kwenda dukani toka asubuhi mpaka sasa usiku hautja muona" .

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela alifika eneo la tukio baada ya kumhoji mzazi akagundua walichelewa kutoa taarifa polisi. Baada ya msako wa muda was saa 3 usiku mtoto alipatikana eneo la Mkungugu km 33 kutoka Iringa Mjini.

Binti wa miaka 14 (Jina linahifadhiwa) alikuwa akitoroka na mtoto huyo gari la polisi la doria likishirikiana na wananchi wa kijiji cha Mkungugu lilifanikiwa kumuweka chini ya ulinzi mtuhumiwa huyo wa wizi wa mtoto.

Mkuu wa Wilaya alifika akiongozana na mama Mzazi wa mtoto pamoja na Diwani wa kata ya Kisinga Mh Ritha Mlagala. Binti mwizi yupo kituo cha polisi akiendelea kuhojiwa na mama mzazi baada ya kuandika maelezo alipewa fomu ya matibabu na kumpeleka mtoto hospitali.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela amekemea vikali kitendo cha uzembe wa mama huyu na wazazi kwa ujumla "pamoja na mama huyu kuwa na uchungu wa mtoto bado ana mashtaka ya kujibu ya uzembe, watu tusiowajua tusiwape watoto wetu hata kidogo huu ni uzembe wa hali ya juu" alisisitiza Mkuu wa wilaya.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni