Penati ya dakika 90 iliyopigwa na
Lionel Messi ilitosha kuizamisha Leganes na kuiepusha Barcelona na
matokeo ya aibu ya mfululizo katika Ligi Kuu ya Hispania, La Liga.
Mbingwa hao watetezi walishuka
dimbani wakiwa na kumbukumbu ya kipigo cha magoli 4-0 katika Ligi ya
Mabingwa Ulaya kutoka kwa Paris St-Germain.
Lionel Messi aliipatia Barcelona
goli la kuongoza kabla ya Unai Lopez kuisawazishia Leganes, lakini
Messi tena akafunga kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 90.
Unai Lopez akifunga goli la kusawazisha na kufanya matokeo kuwa 1-1
Lionel Messi akipiga mkwaju wa penati na kufunga goli la pili
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni