Arsenal imemuepusha kocha Arsene
Wenger kukabiliwa na shinikizo zaidi baada ya kupambana kiume na
kufanikiwa kutinga robo fainali ya Kombe la FA kwa ushindi wa magoli
2-0 dhidi ya Sutton United.
Katika mchezo huo Arsene Wenger
alifanya mabadiliko saba kutoka katika kikosi kilichochapwa magoli
5-1 na Bayern Munich katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa wa
Ulaya hatua ya 16 bora.
Shuti la krosi la Lucas Perez
liliipatia Arsenal goli la kuongoza katika dakika 26 na kisha Theo
Walcott akaongeza goli la pili shuti la karibu dakika kumi baada ya
kipindi cha pili, likiwa ni goli lake la 100 kwa klabu yake.
Kipa Ross Worner akiwa chini baada ya mpira wa krosi ya Luas Perez kutinga wavuni
Mshambuliaji Theo Walcott akifunga goli la pili katika mchezo huo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni