Mashirika ya habari ya kimataifa
yamekasirishwa na hatua ya baadhi ya vyombo vya habari kuzuiwa
kuhudhuria mikutano rasmi ya Ikulu ya Marekani na Afisa Habari wa
Ikulu Sean Spicer.
Vyombo vya habari vilivyozuiwa
mikutano hiyo ya Ikulu ni pamoja na BBC, CNN, the New York Times, the
Guardian, the Los Angeles Times, Buzzfeed, the Daily Mail pamoja na
Politico.
Gazeti la New York Times limesema
hatua hiyo haikubaliki na ni tusi kwa demokrasia, huku BBC ikitaka
kupatiwa ufafanuzi na Ikulu ya Marekani kuhusiana na uamuzi huo
unaokandamiza uhuru wa vyombo vya habari.
CNN wao wamesema jambo hilo
halikubaliki na kuongeza kuwa hivyo ndivyo hufanyavyo utawala wa rais
Trump kujaribu kuvizima vyombo vya habari vinavyoripoti ukweli
wasioutaka.
Marufuku hiyo imetolewa wakati rais
Donald Trump akitoa matamishi ya kuvishambulia vyombo vya habari
akisema habari feki ni adui ya watu.
Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa kwenye mkutano wa habari Ikulu
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni