Timu ya Leicester City imecheza kwa
kiwango kinachoridhisha katika mchezo wao wa kwanza tangu wamtimue
kocha wao Claudio Ranieri na kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi
ya Liverpool.
Kwa matokeo hayo ya mchezo huo wa
Ligi Kuu ya Uingereza Leicester imejikwamua kutoka nafasi tatu za
chini, kupitia magoli mawili kutoka kwa Jamie Vardy na moja la Danny
Drinkwater
Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya
Uingereza walionekana kuimarika mno wakiwa chini ya Craig
Shakespeare anayeinoa kwa muda, ambaye anaiongoza timu hiyo kutoka ya
Ranieri aliyeisaidia kutwaa ubingwa msimu uliopita.
Danny Drinkwater akifunga goli la pili la Leicester City
Jamie Vardy akifunga goli lake la pili katika mchezo huo na kufanya matokeo kuwa 3-1
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni