.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 28 Februari 2017

WAZIRI DK.CHARLES TIZEBA KUFUNGUA KONGAMANO LA WADAU WA KILIMO JIJINI DAR ES SALAAM KESHO

POWA
WAZIRI wa Kilimo ,Chakula,Mifugo na Uvuvi Dk. Charles Tizeba
 
                                                                                        Enles Mbegalo

WAZIRI wa Kilimo ,Chakula,Mifugo na Uvuvi Dk. Charles Tizeba anatarajia kufungua kongamano la siku tatu la wadau wa sera za kilimo kesho jijini Dar es Salaam.

Aidha, kongamano hilo litahudhuriwa na wadau zaidi ya 200 kutoka nchi mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kampuni ya Agricultural Non State Actors Forum (ANSAF), Audax Rukonge, alisema serikali imekusudia kuweka kipaumbele kwenye viwanda vya uchakataji wa mazao ya kilimo.

Kongamano hilo litalenga kuongeza uelewa miongoni mwa watunga sera kuhusu mchango wa kilimo katika kuhamasisha ukuaji wa viwanda Tanzani.

“Wadau watajadili kupata tafsiri halisi ya sekta ya uchakataji mazao ya kilimo katika muktadha wa mageuzi ya viwanda Tanzania,”alisema

Rukonge alisema kongamano hilo limedhaminiwa na USAID, Benki ya Dunia,ANSAF,JICA na wadau wengine ambao wamesaidia kuleta watalamu wakiwamo wakulima, watafiti,wafanyabiashara na watunga sera.

Mratibu wa Jukwaa la Sera ya Kilimo na Mchumi mwandamizi Wizara ya Kilimo, Sophia Mlote alisema kongamano hilo la tatu
litajadili maendeleo ya kilimo nchini ikiwamo kujadili namna ya kutetea sera,sheria,kanuni.

Pia alisema kongamano hilo litajikita katika kujadili juu ya mpango wa kilimo cha mihogo,mikunde, samaki, mazao, usafirishaji pamoja na vifungashio kwa kuwa wazalishaji wengi hawana vifungashio.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni