DAR ES SALAAM, Tanzania, Tarehe 17 Februari, 2017/ -- Huduma dijitali ya kutuma pesa, WorldRemit (www.WorldRemit.com/en/ Cameroon),
inaimarisha huduma zake nchini Tanzania, ili kushughulikia mahitaji
yanayoongezeka ya malipo ya papo hapo nchini, kutoka zaidi ya wananchi
milioni 4 wanaoishi ng’ambo.
Sasa, WorldRemit inatangaza:
- Idadi mpya ya shughuli 10,000 za kipekee zilizokamilishwa mwezi wa Desemba 2016 pekee;
- Ongezeko la kila mwaka la 150% katika mwaka wa 2016, lililotokana na kuongezeka kwa haraka kwa akaunti za Pesa Rununu kuwa njia maarufu zaidi ya kupokea pesa.
Wateja
wa WorldRemit wanaweza kutuma pesa nchini Tanzania kupitia Pesa Rununu
kwa akaunti za Tigo Pesa, Vodacom M-Pesa na Zantel Ezy Pesa, na pia
kuweka pesa kwenye benki na kuchukua pesa taslimu.
Watumaji
wakuu wa pesa za kuingia Tanzania wanajumuisha wahamiaji wanaoishi
Uingereza, Uswidi, Australia, Norwe na Kanada, miongoni mwa nchi
nyingine.
Kupitia
WorldRemit, watu wanaoishi katika zaidi ya nchi 50 wanaweza kutuma pesa
papo hapo kwa njia salama kwenda kwa zaidi ya sehemu 140. WorldRemit,
inayojulikana kama ‘WhatsApp ya Pesa’, imefanya shughuli ya kutuma pesa
kuwa rahisi kama kutuma ujumbe.
Pesa zinazotumwa huchangia sana katika kukuza uchumi wa Tanzania - mwaka wa 2015, nchi hii ilipokea jumla ya milioni $390 kulingana na Banki ya Ulimwengu. Kiasi hiki ni takribani mara kumi zaidi ya kiasi kilichotumwa mwaka wa 2010.
Ismail Ahmed, mwanzilishi na Afisa Mkuu Mtendaji wa WorldRemit, anasema: “Ushirikiano
wa huduma yetu ya Pesa Rununu, ikiwa pamoja na huduma zilizopo za
kuweka pesa kwenye benki na kuchukua pesa taslimu, utawapa Watanzania
chaguo nyingi zaidi.
Hii itasababisha mabadiliko kutoka huduma ghali za
kutuma pesa nje ya mtandao kupitia mawakala wa mitaani hadi huduma za
kasi, za bei nafuu na salama za kutuma pesa kupitia mtandao".
Kwa sasa, wateja wa WorldRemit hufanya zaidi ya shughuli 580,000 za kutuma pesa kila mwezi.
Kusambazwa na APO kwa niaba ya WorldRemit.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni