Chelsea imeendelea kukaza buti
katika mbio za kuchukua makombe mawili Uingereza baada ya jana N'Golo
Kante kufunga goli la pekee la ushindi katika kipindi cha pili katika
mchezo wa FA wa robo fainali dhidi ya Manchester United katika dimba
la Stamford Bridge.
Katika mchezo huo wa jana usiku
kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, alilumbana na kocha wa
Chelsea Antonio Conte pia alishambuliwa kwa lugha chafu na mashabiki
wa Chelsea timu ambayo aliwahi kuiongoza mara mbili.
Kocha huyo mreno alikasirishwa na
kitendo cha kiungo Ander Herrera kutolewa nje zikiwa zimebakia dakika
kumi kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza baada ya kumchezea
rafu kwa mara ya pili Eden Hazard.
Shuti la kiungo Kante katika dakika
ya 51 lilifanikiwa kumaliza jitihada za kipa United David de Gea,
ambaye aliokoa vyema mashambulizi ya Hazard na Gary Cahill kabla ya
mapumziko. Kwa ushindi huo Chelsea itakutana na Tottenham katika
mchezo wa nusu fainali.
Refa akimuonyesha Ander Herrera kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Eden Hazard
Kipa David de Gea akishindwa kuzuia mpira uliopigwa na N'Golo
Kante
Kocha Jose Mourinho na Antonio Conte wakizuiliwa wasidundane wakati wakitupiana maneno makali




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni